Dkt. Mpango amesema kuwa takwimu za utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa juu ya hali ya maambukizi ya VVU, inaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe ndo unaoongoza kwa maambukizi ya VVU, na utafiti huo uliwahusisha watu wenye umri wa miaka 15-49 kwa mwaka 2016-17.
"Kiwango cha maambukizi mapya bado kiko juu kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ikiongozwa na Njombe 11.6%, Iringa 11.2% na Mbeya 9.2%. Mikoa yenye maambukizi ya kiwango cha chini ni Unguja 0%, Kaskazini Pemba 0%, Lindi 0.3%, Manyara 1.8% na Arusha 1.9%.", amesema Dkt. Mpango.
Mara baada ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo Rais Magufuli amewataka wananchi kupuuzia watu wanaotoa takwimu za uongo, na kusema kwamba wenye mamlaka ya kutoa takwimu za taifa ni ofisi ya Taifa ya Takwimu pekee.
Post A Comment: