Mshambuliaji Mbaraka Yusuf wa Azam FC atakwenda kupata matibabu nje ya nchi.
Msemaji
wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema uongozi wa klabu hiyo, baada ya kupata
majibu ya vipimo vyake, kesho ataondoka nchini kwenda Afrika Kusini.
“Majibu
yanaonyesha ameumia meniscus kama ambavyo nilieleza awali. Hivyo
atakwenda Afrika Kusini kesho kwa ajili ya matibabu,” alisema.
Mbaraka aliumia wakati akiitumikia timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wakati akiitumikia katika michuano ya Chalenji.
Awali
kulikuwa na taarifa kwamba Azam FC ilimtelekeza, jambo ambalo baadaye
lilikanushwa na klabu ya Azam FC kwamba imekuwa ikiendelea kufuatilia
hali yake.
Post A Comment: