Kampuni
ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi ya dhahabu ya
Buzwagi na Bulyanhulu imefanya tamasha la ajira kwa kuwakutanisha
waliokuwa wafanyakazi wa migodi hiyo na makampuni zaidi ya 20 kwa ajili
kubalishana mawazo na kupeana mawasiliano na taarifa ili wafanyakazi hao
wapate kazi.
Tamasha hilo limefanyika leo Jumatano
Desemba 20,2017 katika ukumbi wa Umoja uliopo katika mgodi wa Buzwagi
uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa
Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk
Chris Mauki.
Akizungumza wakati wa tamasha
hilo,Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu alisema
lengo la tamasha la ajira lilioandaliwa na Acacia ni kuwaonesha fursa za
ajira waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya Acacia kwa kuwakutanisha na
makampuni mbalimbali katika kipindi cha kuelekea kufunga migodi hiyo.
“Tumekutana hapa ili kuonesha fursa
za ajira kwa wafanyakazi wetu waliobobea katika kazi za migodini, kuna
maisha mengine baada ya mgodi,tumealika kampuni ambayo yanachukua
mawasiliano na CV na kama kuna nafasi za ajira basi watapatia ili maisha
yaendelee nje ya mgodi”,aliongeza Busunzu.
“Tulialika makampuni zaidi ya 40, 15
yalikubali kushiriki,na 11 leo yamehudhuria,lakini pia wafanyakazi zaidi
ya 260 wamehudhuria kwa ajili ya kuonana na makampuni haya,Acacia
inaamini tamasha hili litakuwa na mafanikio makubwa
tuliyotarajia”,alieleza.
Aidha Busunzu alisema kupitia program yao ‘No Harm 2020’
yenye miradi 10,wamekuwa wakitoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa
wafanyakazi wao kuhusu namna ya kuishi baada ya kumaliza muda ajira
mgodini ambapo wafanyakazi 800 katika mgodi wa Bulyanhulu na 600 katika
mgodi wa Buzwagi wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali na ajira.
Kwa upande mgeni rasmi Dk Chris Mauki
ambaye ni Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es
salaam aliipongeza Acacia kwa kuwaandaa wafanyakazi wake kwa kuwapatia
mafunzo ya namna ya kuishi baada ya migodi kufungwa huku akiwataka
kukubali mabadiliko na kuthubutu kufanya kazi nyingine badala ya kukata
tamaa.
“Mnayo nafasi ya kufanya
biashara,kuajiriwa,kujiajiri na kuajiri wengine, ,mnachotakiwa kufanya
ni kujitambua,kukubali mabadiliko,kuwa na nidhamu ya matumizi ya
fedha,muishi maisha ya kuokoa muda,kuweni na mahusiano mema na watu
wanaowazunguka na hapo ndipo mtakubaliana nami kuwa kuna maisha baada ya
mgodi”,aliongeza Dk. Mauki.
Nao washiriki wa tamasha hilo
waliishukuru Acacia kuwakutanisha na makampuni hayo kwani wamewapa
urahisi wa kutafuta kazi kwa kukutana na waajiri moja kwa moja na
kuwapatia taarifa zao (CV).
Nayo makampuni hayo yalisema Acacia ina
wafanyakazi wazoefu na waliobobea katika kazi za migodini hivyo
yanaamini yatapata wafanyakazi wazuri watakaowatumia kwenye makampuni
yao.
“Acacia ni kampuni kubwa ya kimataifa, hii ni sehemu nzuri ya kupata wataalamu wanaojua kazi vizuri”,alisema
Kaimu Meneja rasilimali watu kutoka shirika la Madini la taifa- STAMICO
Lameck Kabeho na Jolene Ngaluko Mtalo kutoka Wakala wa ajira. –CV
People Africa.
Naye Meneja wa Huduma na Mahusiano wa
Acacia, Elias Kasitila alisema mpaka sasa wafanyakazi 3000 wameachishwa
kazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na zoezi la kupunguza
wafanyakazi bado linaendelea katika mgodi wa Buzwagi hivyo idadi
itaongezeka.
Kasitila aliyataja makampuni
yaliyoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni Twiga Cement,Mantrac Tanzania
Ltd,Northern Engineering,SAO Hill,Shanta Gold mine,IMED,LINDAM,CV
People,Junior Construction,Sandvick na STAMICO.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA TAMASHA LA AJIRA
Mgeni rasmi Mkufunzi katika Idara ya
Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki akizungumza
katika Tamasha la Ajira lililoandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji madini ya
dhahabu ya Acacia lililofanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika
mgodi wa Buzwagi na kukutanisha pamoja makampuni zaidi ya 10 na
wafanyakazi zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika mgodi wa Buzwagi na
Bulyanhulu wakati Acacia ikielekea kufunga migodi hiyo.Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Dk Chris Mauki akizungumza katika Tamasha hilo la Ajira.Kulia ni Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu.
Meneja wa migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea lengo la kufanya tamasha la ajira
lililokutanisha pamoja makampuni na wafanyakazi wa Acacia ili kupeana
fursa za ajira. Kulia Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George
Mganza,kushoto ni Dk. Chris Mauki.
Meneja wa migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu Benedict Busunzu akiwasisitiza waliokuwa wafanyakazi wa
Acacia kutumia fursa ya tamasha hilo kutafuta maisha nje ya migodi.
Washiriki wa tamasha la ajira wakimsikiliza Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu
Meneja wa migodi ya Buzwagi na
Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea namna Acacia inavyoendelea kutoa
elimu ya ajira na ujasiriamali kwa wafanyakazi wake ili kujiandaa kuanza
maisha mengine nje ya migodi.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Huduma na
Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila. Wa kwanza kulia ni Meneja Msaidizi
wa Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Allan Bunyan akifuatiwa na Meneja
Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Gordon Surgeon
Washiriki wa tamasha la ajira wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia,
Elias Kasitila akielezea kuhusu tamasha la ajira ambapo alisema zaidi
ya makampuni 40 yalialikwa kushiriki tamasha hilo, makampuni 15
yakakubali kushiriki na leo makampuni 11 yamekutana na wafanyakazi wa
Acacia zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika migodi hiyo.
Kasitila alisema mpaka sasa wafanyakazi
3000 wameachishwa kazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu hivyo
wanafanya jitihada za kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata fursa za
ajira sehemu zingine ili maisha yaendelee
Mtaalamu wa Mawasiliano Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Mary Lupamba akitoa maelekezo kwa washiriki wa tamasha hilo la ajira
Tamasha linaendelea
Washiriki wa tamasha hilo wakiwa eneo la tukio
Tamasha linaendelea
Washiriki wa tamasha wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Tamasha linaendelea
Tamasha linaendelea
Washiriki wa tamasha hilo wakiwa eneo la tukio
Waliokuwa wafanyakazi katika migodi ya
Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika ukumbi wa Umoja katika mgodi wa
Buzwagi kwa ajili ya kutembelea vibanda vya makampuni yaliyoshiriki
katika tamasha la ajira kwa ajili ya kupata mawasiliano na kutoa taarifa
zao (CV) kutafuta fursa za ajira
Waliokuwa wafanyakazi katika migodi ya
Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika banda la shirika la Madini la taifa-
STAMICO,wakisikiliza maelezo kutoka Kaimu Meneja rasilimali watu wa
shirika hilo,Lameck Kabeho
Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakiwa katika banda la Shanta Gold Mine kutafuta fursa za ajira
Hapa ni katika banda la kampuni ya Sandvik,kulia ni aliyekuwa mfanyakazi wa Acacia akiuliza jambo
Mfanyakazi wa Mantrac Tanzania Ltd akimsikiliza kwa makini mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia
Ndani ya ukumbi wa Umoja washiriki wa Tamasha la ajira wakibadilishana mawazo
Kulia Mfanyakazi wa CV People,Jolene
Ngaluko akimsikiliza kwa makini mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia
aliyeamua kupeleka CV yake kwa ajili ya kutafuta fursa za ajira
Wafanyakazi wa CV Peole Africa wakiendelea kukusanya CV kwa kuziweka kwenye Laptop
Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakiangalia CV walizokuja nazo kwenye tamasha la ajira kwa ajili ya kuzikabidhi kwenye makampuni
Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakibadilishana mawazo
Meneja Msaidizi wa Ulinzi katika mgodi
wa Buzwagi Allan Bunyan (kulia) na Meneja Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi
Gordon Surgeon wakifurahia jambo katika ukumbi wa Umoja wakati wa
Tamasha la ajira
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog