• Watu 26 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha aliyewafyatulia risasi waumini katika kanisa moja lililopo jimbo la Texas nchini Marekani wakati wa ibada iliyofanyika jumapili.
    Gavana wa jimbo hilo, Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema kuwa hilo ni tukio baya zaidi la mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya Texas
    “Ni majonzi makubwa kwa wafiwa hili ni tukio ambalo halivumiliki ambalo limetokea, nawapa pole sana kwa wafiwa na huu ni msiba wa taifa, hivyo tunaungana kwa pamoja katika majonzi haya,”amesema Gavana Greg
    Aidha, Rais Donald Trump, ambaye yuko ziarani Asia, amesema kuwa tukio la shambulizi hilo halivumiliki na kwamba Wamarekani wanatakiwa kupinga kila kitu kinachihusiana na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.
    Hata hivyo, Mauaji hayo yametokea mwezi mmoja tu baada ya mshambuliaji mwingine kufyatulia risasi watu waliokuwa wakihudhuria tamasha ya muziki Las Vegas na kuwaua watu 58 pamoja na kujeruhi mamia wengine, katika kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutumia bunduki katika historia ya Marekani nyakati za karibuni.
    Share To:

    msumbanews

    Post A Comment:

    Back To Top