Bilionea wa nyumba za Lugumi aliyeteka vichwa vya habari siku za hivi karibuni, Dk. Louis Shika, amekamilisha malipo ya bima kwa ajili ya kutumiwa fedha zake kutoka nchini Urusi..

Dk. Shika aliingia matatani baada ya kushinda mnada wa uuzwaji wa nyumba za Said Lugumi hali iliyosababisha kukamatwa na polisi, lakini binafsi alisisitiza kuwa fedha hizo anazo na sasa anaelekea kuthibitisha hilo kwa kufanya mchakato wa kutumiwa fedha.

Waandishi wa habari walimkuta Dk. Shika akiwa katika huduma za mtandao wa internet katika shirika la Posta Jijini Dar es Salaam, ambao walikuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye na kujikuta hata mwenyewe akimshangaa bilionea huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutuma taarifa za miamala hiyo, Dk. Shika amesema ametuma kiasi cha dola 100 ambapo anatarajia muda si mrefu ataweza kutumiwa fedha zake na kwenda kulipia asilimia 25 ya fedha zinazotakiwa katika nyumba hizo.
Alipoulizwa kama fedha hizo zikichelewa na kukuta mchakato huo wa malipo umepita, amesema kwa kujiamini, atanunua nyingine kwani Dar es Salaam kuna nyumba nyingi zinazouzwa siyo lazima hizo za Lugumi.

Kiasi hicho cha fedha, amekilipa kwa kwa Benki ya Equity kwenda Benki ya Bankok nchini Thailand, mchakato utakaomwezesha kutumiwa fedha zake na kuweza kununua nyumba hizo.

Katika hatua nyingine Dk. Shika alisifia huduma za shirika hilo na kueleza kwamba ndiyo hutuma huduma za internet katika kutuma nyaraka zake mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: