Tarehe 02 Novemba 2017, Chama cha ACT Wazalendo kilipokea wito toka kwa
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wa kuwataka Wajumbe wote wa
Kamati Kuu ya ACT Wazalendo wafike Kituo cha Makosa ya Fedha (Financial Crime
Unit) kilichopo Maeneo ya Kamata, Kariakoo Jijini Dar es salaaam kwa ajili ya
mahojiano siku ya Jumatatu tarehe 6 Novemba 2017.

Ikumbukwe kuwa wito huu unakuja baada ya Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe

kuhojiwa katika kituo hicho kwa takribani masaa matatu siku ya tarehe 31 Oktoba 2017

kutokana na Taarifa ya Chama Kuhusu Kusinyaa kwa Uchumi.

Uamuzi huu wa Kuihoji Kamati Kuu nzima unashangaza sana kwa sababu mbili;

i. Kamati Kuu ni chombo cha kitaifa Cha Chama chenye mamlaka ya kufanya
maamuzi kwa mujibu wa katiba ya ACT Wazalendo kama chombo na si kama
mjumbe mmoja mmoja;
ii. Jeshi la Polisi halina madaraka ya kushughulikia wala kuingilia maamuzi halali ya
vyombo (organs) katika vyama vya siasa.
Tangu tuzindue kampeni zetu katika kata ya Kijichi, Jeshi la Polisi limefanya maamuzi

ya kushikilia au kuhitaji kuwahoji viongozi, ambayo kwa namna moja au nyingine
yanaathiri kampeni zetu.
Kwa maamuzi haya ya Jeshi la Polisi, wiki sasa inakatika viongozi wetu wakilazimika
kusalia Dar es salaam kusubiri kuhojiwa na Polisi. Tutaendelea na kampeni kama
kawaida. Polisi watafute namna na wakati sahihi wa kufanya mahojiano na viongozi
wetu.
 Tunawaomba viongozi, wanachama wa ACT Wazalendo na wananchi kwa ujumla
kuendelea na kampeni za udiwani wakisisitiza ujumbe wetu wa UCHUMI na HAKI.

Yeremia Kulwa Maganja,
Kaimu Mwenyekiti wa Chama,
ACT Wazalendo.

Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2017.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: