Na  Ferdinand Shayo,Arusha.


Jumla ya Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo  katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha Hanifa Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni wengi.

Kwa upande wao Wanufaika wa Mikopo hiyo kwaniaba ya Walemavu Mwajuma Juma  na Patrick Petro  wameishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: