Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amejitolea kumsaidia Kijana Ahmed Albaity anaesumbuliwa na tatizo la Uti wa Mgongo lililompelekea kulala kitandani kwa takribani miaka 10.
Ahmed Albaity anatakiwa kwenda kutibiwa Nchini China kwa muda wa Wiki tatu akiambatana na Wasaidizi Wawili ambapo Gharama za Matibabu zinazohitajika ni zaidi ya Dola 40,000 za Marekani ambapo Sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha Dolla 27,000.
Makonda amesema atafanya jitihada zote kuhakikisha Ahmed anapatiwa Matibabu ili aweze kupona na kutimiza ndoto zake akiwa na Afya Njema.
Mapema leo Makonda ametembelewa Ofisini kwake na Balozi Mpya wa China Nchini Tanzania Wang Ke ambae amekuja kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa ambapo katika Mazungumzo Makonda amemgusia Balozi huyo Suala la Matibabu ya Ahmed Albaity ambapo Balozi Wang Ke alieambatana pia na Daktari Bingwa wa China aliebaki Nchini kwaajili ya Shughuli ya Serikali ya China ambapo wamemtazama na kupitia Ripoti ambapo wameahidi kulifanyia kazi suala hilo 
Katika Mazungumzo hayo pia wamejadili Masuala mbalimbali ikiwemo Kuimarisha Usalama, Kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu na kuongeza huduma kwa Wananchi.
Makonda pia ameishukuru Serikali ya China kwa kuleta Meli ya Jeshi la China yenye Hospital ndali ambayo imesaidia kutoa vipimo na Matibabu kwa wananchi wengi.
Kwa Upande wake Bolozi Mpya wa China Nchini Tanzania Wang Ke amesema Serikali ya China itaendelea kusaidiana na Tanzania katika masuala yote ya maendeleo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment:

Back To Top