Mkurugenzi wa jiji la Arusha mhe: Athumani Kihamia leo amefanya ziara ya ya kutembelea na kukagua thamani ya fedha (Value for money) katika miradi ya  afya inayoendelea kutekelezwa na jiji la Arusha.

Miradi aliyoitembelea nia pamoja na mtaro wa kusafirisha maji machafu wenye urefu wa km1.2 eneo la dampo la kisasa la takataka la Murieti uliopo katika hatua za ukamilishwaji, Kituo cha afya cha Murieti ambacho kipo katika hatua ya upauaji,  kituo cha polisi na nyumba za askari Murieti, Kituo cha afya cha  Moshono ambacho kimeezekwa bati hivi majuzi,  pamoja na  ujenzi wa zahanati ya Olimoti ambayo ipo hatua ya usafi baada ya kukamilika

Mkurugenzi Kihamia amesema ameridhishwa sana na ujenzi wa miradi hiyo na ameahidi kuisimamia kwa karibu zaidi ili ifaidishe wananchi hasa wenye kipato cha chini.'kukamilika kwa miradi hii ni mafanikio ya utekelezaji wa ahadi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli pamoja na ilani ya CCM ya 2015 hadi 2020
Share To:

msumbanews

Post A Comment: