Arusha,Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro amefika Leo katika kituo kikuu cha polisi cha kati kuwajulia hali wafuasi 12 wa Chadema wanaoshikiliwa na jeshi la polisi .
Mbali na kuwajulia hali wafuasi hao Lazaro amelitaka jeshi hilo kuwafikisha mapema watuhumiwa wote mahakamani ili haki iweze kutendeka.
Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi Mara baada ya kuwajulia hali wafuasi hao alisema kwamba amefanikiwa kukutana nao wote na wanaendelea na afya njema.
Lazaro,alisema kwamba amefanikiwa kuzungumza na baadhi ya viongozi wa polisi kituoni hapo ambapo aliwaeleza kwamba wawafikishe watuhumiwa hao mapema kesho mahakamani .
Alisema kuwa polisi wamemjibu kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani na kuwaondoa hofu wanachama wa chama hicho mkoani hapa kwamba wapo imara na wanaendelea na afya njema
Hatahivyo,alitoa wito kwa jeshi la polisi kuacha kukibeba chama tawala katika uchaguzi mdogo wa udiwani unaotaraji kufanyika mwezi ujao na kusema kwamba waache vyama vya siasa vipambane kwenye uwanja wa kisiasa.

Post A Comment: