Leo November 9, 2017 huko Arusha Mchungaji Baltazar Yae wa Kanisa la Bethel Grace Church Mission Tanzania la Jijini Arusha, ameamua kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo huku akitoa sababu mbili zilizopelekea uamuzi wake huo.
Ameeleza kuwa sababu yake ya kwanza ni kwamba amefurahishwa na siasa za masuala za chama hicho akisema kinamgusa moja kwa mojaMtanzania. Pili amefurahishwa na mkazo wanaoutoa kwenye kilimo na namna wanavyopambana kupigania hali za maisha ya Watanzania.
“Ninajiunga na Chama hiki nikiamini hili ni jukwaa muafaka kushiriki siasa za Arusha na nchi. Nina imani kupitia Chama hiki nitatoa mchango wangu kwa Taifa.” – Mchungaji Baltazar Yae
Share To:

msumbanews

Post A Comment: