Siku kadhaa baada ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Samwel Nyalandu kutangaza kukihama Chama Cha CCM kwa madai kimepoteza mwelekeo na kushindwa kuikosoa serikali, Kada wa chama hicho aitwaye Methusela Gwajima, amemjibu mwanasiasa huyo kwa kumwambia sababu alizotoa ni za kitoto sambamba na kueleza baadhi ya mafanikio na mambo ambayo yamefanywa na serikali hiyo inayoongozwa na chama cha CCM.


Hata hivyo kada huyo ameweka wazi kuwa huenda kilichomuondoa Nyalandu ni baada ya kusikia kuwa anachunguzwa tuhuma za mambo aliyofanya akiwa Waziri wa mali asili na utalii na kwamba ameshindwa kusubiri kuumbuliwa kwakuwa yalikiaibisha Chama cha mapinduzi na kuitia Nchi hasara.

 TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI
Share To:

msumbanews

Post A Comment: