Kampuni ya Good One leo wametoa msaada wa mifuko ya cement 200 ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Mkonda za ujenzi wa ofisi na nyumba  za walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja masoko wa kampuni hiyo Thomas Ma amesema kuwa wametoa msaada huo kwa lengo la kufanikisha harakati za mkuu wa mkoa za kutaka walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri na yaliyo bora.

Kwa upande wake  makamu mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu Dar es salaam ACP Solomon Urio ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo.

"Hiki ni kielelezo tosha kwamba mkuu wa Mkoa anafanya kazi nzuri na ipasavyo na ndio maana wananchi wake wanaendelea kumuunga mkono kwa kila hatua, makampuni na watu binafsi wanaendelea kutoa misaada" alisema ACP Solomon.

Kufuatia misaada hiyo ofisi zinaendelea kujengwa sehemu mbalimbali katika wilaya zote tano, hivyo wadau na watu mbalimbali waendelee kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: