Kampuni ya Global Publishers imeandaa Tamasha maarufu kwa jina la ” USIKU WA 900 ITAPENDEZA”, litakalofanyika Desemba, 9 mwaka huu katika ukumbi wa DAR LIVE uliopo Mbagala Jijini Dar es Salaam.
Katika tamasha hilo, Dkt. Shika atapata nafasi ya kuzungumza na watanzania kuhusu maisha yake kwa ujumla na namna ambavyo anakusudia kutumia utajiri wake kuwasaidia watanzania.
Akiongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Meneja wa Ukumbi huo, Rajab Mpeta alisema kuwa, tamasha hilo lintarajiwa kuanza saa 11 jioni ambapo watu zaidi ya 400 wanatarajiwa kuhudhuria.
Akifafanua zaidi alisema, mgeni rasmi katila tamasha hilo anatarajiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ambapo pia burudani mbali mbali zitakuwepo ili kukonga nyoyo za wapenzi.
Alitaja baadhi ya burudani zitakazokuwepo kuwa ni pamoja na vikundi vya uchekeshaji, kikundi cha Taarab cha Jahaz, Bendi ya muziki ya Twanga Pepeta, msanii Juma Nature pamoja na wasanii wengine ambapo kiingilio cha kawaida kitakuwa Sh.5,000 na VIP Sh.15,000.
Post A Comment: