Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kassim Majaliwa amekitaka Chuo kikuu Hiria nchini kuhakikisha kinaongeza ubora wa utoaji Elimu na kupanua wigo wa udahili kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 33 ya Chuo hicho ambayo yamefanyikia mkoani Singida na kusisitiza kuwa Umuhimu wa Chuo kikuu huria uko bayana katika kuhakikisha malengo ya serikali ya kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda inafikiwa kupitia wataalamu wanaomaliza chuoni hapo.


Waziri Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya Tano inatambua na inaunga mkono juhudi zinazofanywa na uongozi wa chuo hicho huku wakisisitizwa kuzingatia vigezo, taratibu za utoaji wa Elimu iliyo bora ili wapatikane wataalamu ambao ni bora kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali inatambua mchango wa Chuo hicho katika kipindi cha miaka 25 ambapo kimekuwa kikitoa  Elimu katika masafa ya mbali hali ambayo inahitaji mwanafunzi kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili kifikia malengo.

Kutokana na juhudi hizo Waziri Ndalichako ameahidi Serikali itaendelea Kuimarisha miundombinu ya Tehama ili Elimu hiyo ya masafa iweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Waziri Ndalichako amewataka wahitimu kutumia vyema ujuzi na kuhakikisha wanaimarisha utendaji kazi katika serikali na hata Sekta binafsi.

Pia amewataka wahitimu kujenga nadhani pamoja na kuwa na ari katika  uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi katika Shughuli ambazo watakuwa wanazifanya.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

30/11/2017
Share To:

msumbanews

Post A Comment: