Chama cha mapinduzi (CCM) Arusha kupitia kwa katibu Elias Mpanda kimefunguka kuhusu Wafuasi wanaodaiwa kuwa wa CHADEMA kuwashambulia watu watatu wa CCM akiwemo Mgombea Udiwani kata ya murieti Fransis Mbise.
Mpanda amesema “Sisi CCM kwakweli ni Wastaarabu na ninataka niwahakikishie kati ya kata zote 8 ambazo nimesema tutashinda, tutashinda kwasababu tuna hoja za kusema juu ya Wananchi“
“Nashukuru Wananchi wa Arusha na kama sio Tanzania nzima wameshatambua dhamira kubwa ya CHADEMA kwamba dhamira yao sio kuwaletea Wananchi maendeleo bali kuwatumia kwa maslahi yao binafsi”
“Ushauri wa bure kwa ndugu Godbless Lema, kwanza Wafuasi wa CHADEMA niwaombe sana wasitumike vibaya kwasababu hata jana walioleta fujo wote walikamatwa na wako polisi lakini Godbless alikimbia pamoja na katibu wa chama wa Wilaya”
Post A Comment: