Jana
October 18 2016 kulifanyika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika
hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Burka nje kidogo ya jiji
la Arusha, lakini shughuli hiyo ilisimama baada mbunge wa jimbo la
Arusha mjini Godbless Lema kusimama kupinga maelezo yaliyokuwa
yakitolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Maelezo
ya RC Gambo yalisema kwamba eneo la mradi ule limetokana na maono
aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala, maelezo ambayo mbunge
Lema alikuwa akiyapinga na kudai yeye amehusika kutafuta ardhi na
wafadhili, Lema alidai maelezo hayo yamejaa upotoshwaji na siasa ndani.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini.
Leo
October 19 2016, mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha
ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa facebook ametoa
ushauri kwa RC Gambo na Mbunge Lema, Zitto amesema…..…
"Nakasirishwa
sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa
Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya
mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi.
"Kaa
Na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya.
Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi
kufutika kirahisi.
"Nakushauri
kaa chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa
pamoja. Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio
hekima."-Zitto Kabwe
Zitto Kabwe
Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo
una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu
nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. Kaa Na Mbunge Godbless Lema mnywe
kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza
munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa
chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja.
Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.
Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.
Post A Comment: