WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amefunga Tamasha la shindano la Nyimbo za Jadi Rungwe na kuonesha kufarijika na mwitikio mkubwa.
Tamasha hilo ambalo lilifanyika kwa siku mbili kati ya Oktoba 7 na 8 mwaka huu likihusisha halmashauri tatu za Kyela, Rungwe na Busokelo.
Waziri Nape alisema mahudhurio na mwitikio wa tamasha hilo umeimsha Serikali hivyo kuona ni vema kila Wilaya na Mkoa kufanya matamasha kama hayo hadi kufikia ngazi ya Taifa.
Aidha alienda mbali zaidi na kupendekeza uwanja wa Tandale ulipo Tukuyu mjini ambao ulitumika kwa ajili ya Tamasha kubadilishwa jina na Kuitwa Dk. Tulia jambo ambalo liliungwa mkona na wananchi zaidi ya 10,000 waliohudhuria.
Alisema washindi katika matamasha hayo watasaidia kutangaza mila na desturi za Watanzania, vivutio vya utalii vinavyopatikana nchiniikiwa ni pamoja na kutengeneza fursa ya ajira kwa vijana.
Kwa upande wake Dk. Tulia alisema katika Tamasha hilo Vijana 20 watasomeshwa katika Chuo cha Sanaa bagamoyo kwa ngazi ya awali ya miezi miwili huku vijana 5 watachaguliwa kwenda kusomea cheti ambao watakuwa wana elimu ya kidato cha nne huku vijana wawili waliohitimu kidato cha sita wakisomea ngazi ya diploma.
Kwa upande wao majaji wa Tamasha hilo wakiongozwa na Ismail Michuzi Mwasulimo waliwataja washindi wa tamasha hilo kuwa ni upande wa Ling’oma na zawadi zao kwenye mabano kuwa ni Mbagamoyo kutoka Kyela msindi wa kwanza (750,000), mshindi wa pili Lupaso (500,000) na mshindi wa tatu ni Njisi (350,000).
Ngoma ya pili ni Ling’oma aina ya kituli mshindi wa kwanza Kasanga(750,000), mbamila na Mshindi wa tatu ni Kakindu.(zawadi zote ni sawa kwa kila aina ya ngoma kwa mshindi wa kwanza 750,000, pili 500,000 na tatu ni 350,000).
Upande wa Samba ulichukuliwa na Mshindi wa kwanza Katumba, Pili Mpunguti na tatu Sumu ya Mamba huku maghosi mshindi wa kwanza akiwa ni Kyatasumo, pili Ilopa na tatu ni Songela.
Ngoma ya Ndingara mshindi wa kwanza ni Lukwego, pili Mwambula na tatu ni Itagata huku ngoma ya kitumbwike ikiwa na mshiriki mmoja ambaye ni Ndobho aliyepata shilingi 350,000.
Kwa upande wa Lipenenga mshindi wa kwanza ni Iponjola, pili Bugoba na tatu ni Ipuguso huku upande wa Kibhota akiwa mshiriki mmoja ambaye pia ni Iponjola aliyepata 350,000.
Ngoma ya Kapote washindi ni kwanza Usweghe Mwambapa, pili Asamisye na tatu ni Mwandulusya huku ngoma ya Kimwenge akiwa mshiriki mmoja ambaye ni Balenga Balandani waliojipatia shilingi 350,000.
Post A Comment: