Home
Kitaifa
WATUMISHI WA UMMA SHEREHE ZA MWENGE SIMIYU WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Baadhi ya
Watumishi wa Umma wakiendelea kupata huduma ya usajili na Utambuzi
katika viwanja vya Sabasaba ambako maonesho ya kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru yanafanyika. Wakati wa zoezi hilo mbali na kjaza fomu za
maombi ya Vitambulisho, watumishi hao wamepata fursa ya kupigwa Picha,
kuchukuliwa alama kumi (10) za vidole pamoja na saini ya Kielektroniki
na hivyo kuwa wamekamilisha taratibu zote muhimu za usajili
Mmoja wa
Watumishi akiendelea na taratibu za usajili na kuchukuliwa alama za
kibaiolojia wakati wa usajili watumishi wa Umma, zoezi linaloendelea
mkoani Simiyu
Mmoja wa
Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ofisi ya Wilaya ya
Bariadi (mwemye kofia nyeupe), akiendelea kuingiza taarifa za mmoja wa
Watumishi wa Umma aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la Usajili
watumishi wa Umma likiendelea mkoani Simiyu. Wengine waliomzunguka ni
Watumishi kutoka Idara, Taasisi na Wizara za Serikali wakiendelea
kusubiria huduma hiyo
Akiweka
saini ya kielektroniki kwenye kifaa maalumu cha kukusanya taarifa wakati
wa zoezi la Usajili ni mmoja wa maafisa afya katika Mkoa wa Simuyu
ambaye alikuwa miongoni mwa watumishi waliojitikeza kusajiliwa
Vitambulisho vya Taifa sambamba na maadhimisho ya kilele cha sherehe za
Mwenge
Watumishi
wa Umma mkoani Simiyu; wamekuwa miongoni mwa watumishi waliojitokeza
kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa katika zoezi linaloendelea
kote nchini, pamoja na kusherehekea kilele cha mbio za Mwenye wa Uhuru
zinazoadhimishwa kitaifa mkoani Simuyu. Kilele cha sherehe hizo ni
Octoba 14,2016 sherehe zitakazoambatana na kumbukumbu ya Hayati Baba wa
Taifa; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Miongoni
mwa watumishi wanaoendelea na Usajili katika mabanda maalumu ya
maonyesho mkoai humo; ni Walimu na watumishi wengine kutoka sekta ya
Afya, WIzara, Wakala na Taasisi za Serikali
Wakizungumza
wakati zoezi hilo likiendelea; mbali na kupongeza elimu kwa umma
inayoendelea kuhusu namna zoezi la Usajili ili na Utambuzi
litakavyoendeshwa nchi nzima, watumishi hao wamepongeza jitihada kubwa
za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa
kutofumbia macho matatizo ya watumishi na hasa jitihada zake katika
kupambana na watumishi hewa.
“ iwapo
kweli mfumo huu utatumika vile tunavyoelezwa kwa hakika shughuli za
utendaji Serikalini zitaboreshwa sana hususani masuala yanayohusu
maslahi ya watumishi na kuondokana kabisa na watumishi wachache ambao
kwa udanganyifu wao wamepelekea sisi watumishi wa Umma kutothaminiwa na
jamii” walisisitiza baadhi ya watumishi waliozungumza na NIDA wakati
zoezi hilo likiendelea
Kwa
upande wa wananchi wengi wameonyesha kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu
faida za kuwa na Vitambulisho vya Taifa, na mfumo wa kielektroniki
utakaounganishwa na mifumo mingine ya Serikali ingawa baadhi
wamesisitiza bado elimu kwa umma kuhusu Vitambulisho inahitajika
hususani kwa wananchi walioko vijijini
Sherehe
za mwaka huu za kilele cha mbio za Mwenge Kitaifa, zimekwenda sambamba
na maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi, Masharika
na Wakala za Serikali; katika kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi
katika shughuli za maendeleo
Back To Top
Post A Comment: