Mwakilishi
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Boniface Temba (katikati) akiwa
katika kikao cha wadau wa maji kuhusu kuhusu kuhuisha mipango ya maji
Mkoa, Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta Abdalah
Dihenda na kushoto kwake ni Mhandisi wa Maji kutoka Sekretariet ya Mkoa
Emaeli Nkopi.
Kikao cha
wadau wa maji Mkoa wa Singida kikiendelea mweye tai nyekundu ni Afisa
Afya Mkoa wa Singida Habib akiwa na kushoto kwake ni mkurugenzi wa
mpango wa Water Aid Tanzania Abel Dugange.
Wadau wa Maji Mkoa wa Singida wakiendelea na kikao.
Wadau wa Maji Mkoa wa Singida wakiendelea na kikao.
Na Grace Singida.
Serikali
na wadau mbalimbali wanatakiwa kuunganisha nguvu na kuzielekeza katika
kuelimisha jamii juu ya athari za uchafu ili wahamasike na kuupinga kwa
kujenga vyoo bora, kutumia maji safi na salama na kutumia huduma za
usafi wa mazingira.
Ari hiyo
imetolewa na Mkurugenzi wa Mpango wa ‘Water Aid’ Tanzania Bw. Abel
Dugange wakati wa kikao cha wadau wa maji wakati wa kuhuisha mipango ya
sekta ya maji ya Mkoa wa Singida.
Dugange
amesema nguvu kubwa inatakiwa ielekezwe katika kutoa elimu kwa jamii ili
wajenge vyoo bora na kuvitumia, watumie maji safi na salama ili
kujiepusha na magonjwa mbalimbali yatokanayo na uchafu.
Ameongeza
kuwa serikali inapoteza fedha nyingi katika kuwatibu wananchi wanaogua
magonjwa kama kipindupindu, kuhara pamoja na ukusanyaji na utekezaji wa
uchafu huku wananchi pia hupoteza pesa kwa kujitibu huku wakipoteza muda
wa kuzalisha mali kwenye matibabu.
Dugange
amesema mpango wa ‘Water Aid’ kwa mwaka 2016 mpaka 2020 utalenga
kuunganisha nguvu na kusaidiana na halmashauri katika kutekeleza mipango
yao ya sekta ya maji na usafi wa mazingira ili kufikia malengo ya
kitaifa katika sekta hiyo.
Amesema
kwa tafiti za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa asilimia 58 ya watanzania
hupata na kutumia maji safi na salama huku asilimia 18 tu hutumia huduma
za usafi wa mazingira.
Dugange
amesema kwa upande wa upatikanaji na matumizi ya vyoo bora vya kwa Mkoa
wa Singida mijini ni asilimia 31 wakati vijijini ni asilimia nane.
Katika
majadiliano hayo wahandisi wa maji na maafisa mazingira wa halmashauri
walitoa changamoto za sekta hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa hasa
vya usafiri wa kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali.
Changamoto
nyingine ni pamoja na visima vingi vya vijijini kuchimbwa maeneo ya
mashamba ya wanakijiji ambapo hawalipwi fidia na kusababisha uharibifu
wa vyanzo na visima vya maji hasa ukataji wa miti.
Kumekuwepo
na wizi wa vifaa katika miradi ya maji hasa solar huku wanakijiji
wakiomba kuwekewa umeme wakati utunzaji wa miradi hiyo wakishindwa
kuchangia huduma hizo.
Kwa
pamoja wadau wamekubaliana kuunganisha nguvu katika kutatua kero za
upatikanaji wa maji pamoja na kuboresha usafi wa mazingira
Post A Comment: