WANANCHI WAJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUMUUA KIJANA MMOJA
ANAESADIKIKA KUWA NI MMOJA WAPO WA KUNDI PANYA ROAD MBAGALA JIJINI DAR ES
SALAAM
'
Samahani kwa kutumia picha hii nia ya kuitumia ni kujaribu kuonesha
changamoto ilivyo kwa vijana hawa wanaopoteza maisha kwa kujihusisha na
kundi hilo la panya road'
Wananchi
wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la
panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem
Dar es Salaam leo jioni. Katika tukio hilo vijana wengine wawili
walipoteza fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.
Wananchi wakiangalia mwili wa kijana huyo (haupo pichani)
Wananchi
wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la
panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem
Dar es Salaam leo. Katika tukio hilo vijana wengine wawili walipoteza
fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.
WANANCHI
wa Mbagala sabasaba wamemuua kwa kumshambulia kwa mawe na kisha
kumchoma moto kijana mmoja anayedaiwa kuwa ni mharifu wa kundi la panya
road ambaye alikuwa na wenzake zaidi ya 15 ambapo wawili kati yao
walipoteza fahamu kutokana na shambulio hilo.
Tukio
hilo la kushambuliwa kwa panya road hao lilitokea majira ya saa 11
jioni katika eneo la Mbagala Sabasaba baada ya vijana hao kukurupushwa
walipokuwa wakikimbia walipokuwa wakifanya uhalifu maeneo ya sabasaba
Magengeni na Mbagala Zakhem.
Polisi
waliofika eneo la tukio walilazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya
wananchi ili waweze kuuchukua mwili wa kijana huyo ambaye hakufahamika
jina lake.
Akizungumza
na mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ambaye alijitambulisha kwa
jina moja la Khalfan alisema usalama wa wananchi upo mashakani kufuatia
kundi hilo la panya road.
"Hawa
panya road walikuwa zaidi ya 15 wakitokea Mbagala Zakhem ambako
walikuwa wakikimbizwa na wananchi baada ya kufanya uhalifu na walipofika
hapa Sabasaba walizingirwa na wananchi ambapo watatu kati yao walianza
kushambuliwa na mmoja kupoteza maisha baada ya kuchomwa moto " alisema.
Alisema
vijana wawili kati yao walijeruhiwa vibaya na kupoteza fahamu lakini
wenzao wengine walifanikiwa kukimbia kuelekea maeneo ya Yombo Dovya huku
wakiahidi kurudi kulipiza kisasa kufuatiwa kuuawa kwa mwenzao.
Mkazi
mwingine wa Mbagala kwa Mangaya aliyejitambulisha kwa jina { Tumelihifadhi } alisema vijana hao wataendelea kuuawa na wananchi kwa kuwa kila
wanapokwenda kutoa taarifa polisi hawachukuliwi hatua yoyote badala yake
uachiwa na kurudi mitaani kuendeleza uhalifu wao" alisema Mwarami.
Aliongeza
kuwa kutokana na kuwa na umri mdogo wanashindwa kupelekwa kwenye
mahakamani kutokana na kulindwa na sheria ya utoto jambo linalowatia
hasira wananchi na kuamua kujichulia hatua mkononi na kuanza kuwaua.
Alisema vijana hao wamekuwa wakitokea maeneo ya Kitunda, Moshi Baa na Yombo kwenda kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Gilles
Muroto alipopigiwa simu jana jioni ili kuzungumzia tukio hilo alisema
alikuwa kwenye mkutano hivyo apigiwe baadae.
Hata
hivyo jeshi la polisi mara kadhaa limekuwa likataa kuwepo kwa kundi
hilo la panya road likieleza kuwa wao wanawahesabu kama walivyo wahalifu
wengine wa matukio ya ujambazi na mengine
Post A Comment: