Home
Kitaifa
WANAFUNZI 196 WANUSURIKA KUFA KWA MOTO BWENINI MKOANI PWANI
WANAFUNZI wasichana wapatao 196 wa shule
ya sekondari ya Moreto iliyopo kata ya Lugoba tarafa ya Msoga Jimbo la
Chalinze mkoani Pwani, wamenusurika kufa baada ya bweni lao kuteketea
kwa moto jana asubuhi.
Mbunge
wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa msaada ya magodoro 50 yenye
thamani ya Sh milioni 2.2 kwa kuwa mali zote wasichana zimeteketea.
“Tumshukuru
Mungu pamoja na kutokea kwa hasara ya kuteketea kwa mali, lakini hakuna
madhara kwa wanafunzi yaliyotokea,” amesema Ridhiwani.
Amewapa pole walimu na wanafunzi na kuwaomba wadau wengine, kujitokeza kwenda kusaidia pale watakapojaaliwa.
Mkuu
wa Shule hiyo , Justine Lyamuya, amesema, ajali hiyo ni ya Oktoba 5,
asubuhi ambako walianza kuona moshi mzito katika bweni mojawapo
wanaloishi wasichana wa shule hiyo.
Alisema wakati moto huo unazuka, wanafunzi hao walikuwa kwenye masomo yao darasani.
"Tulifuatilia
na kukuta moto umeshashika kwenye bweni hilo na jitihada za kuuzima
zilishindikana,” alisema Lyamuya na kuongeza kuwa mali zote za wanafunzi
wanaolala kwenye bweni hilo zimeteketea kwa moto hivyo kwa sasa
wanafanya tathmini kujua kiwango cha hasara.
Polisi mkoani Pwani inafanya uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Boniventure Mushongi amesema, jengo hilo linatumia nishati ya umeme wa jua.
Amesema uchunguzi wa kina utafanyika kujua kiini cha kuzuka kwa moto huo.
Amesema bweni hilo linakadiriwa kuwa na wanafunzi 196.
Kamanda Mushongi amesema thamani za mali za wanafunzi zilizoteketea katika moto huo, bado haijafahamika.
Chanzo-Habarileo
Kama Una Habari,Picha,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255762 561 399
Back To Top
Post A Comment: