Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Mkoani Mwanza, Peter Saramba
na Mpigapicha Michael Jamson wamepata ajali eneo la Kimbu B, Wilaya ya
Bariadi wakiwa wanatoka Simiyu kwenye sherehe za maadhimisho ya
kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere
zilizoambatana na kuzima mwenge.
Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya ajali hiyo, Saramba
alisema watu wawili wamefariki papohapo katika ajali hiyo wakati yeye
akiwa amelazwa katika hospitali ya Mkula Wilaya ya Busega akipatiwa
matibabu kufuatia majeraha aliyoyapata..
“Ajali ilikuwa mbaya sana,ila namshukuru Mungu nipo mzima ingawa
nimepata majeraha madogomadogo, lakini tumeletwa hapa Busega katika
hospitali ya Kikula kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na tayari madaktari
wanatuhudumia hapa” alisema Saramba.
Back To Top
Post A Comment: