CHAMA cha waandishi wa
habari mkoa wa Njombe kimesema kuwa kinaungana na viongozi wengine wa vyama vya
habari hapa nchini ili kuishawishi kamati ya bunge kuto upitisha Muswada wa
sheria ya huduma za habari ili kuusogeza mbele na kuwapa waandishi wa habari
kuujadili kwa kina.
Muswada huo unatarajia kupitishwa na bunge linalotarajiwa
kuanza Mwishoni mwa Oktoba ambapo mpaka sasa Baadhi ya waandishi mikoani
hawajaupitia na hawajatoa maoni yao.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Njombe Khamis Kasapa amesema kuwa muswada huo ukipitishwa
unamaslahi kwa waandishi wa habari licha ya baadhi ya vipengele kuwabana
waandishi.
Post A Comment: