SHIRIKA
la kimataifa la British Council limesema vijana wengi nchini Tanzania wanaishi
wakiwa na hofu na mashaka kutokana na kutokuwa na uhakika wa kuweza kuzitimiza
ndoto zao kunakotokana na ukosefu wa ajira, mitaji na uelewa mdogo wa fursa
zinazopatika serikalini.
Akizungumza
kwenye kongamano la kupaza sauti lililowakutanisha vijana zaidi ya 150 wa
Dodoma mjini katika ukumbi wa Saint Gasper Mkurugenzi wa Mipango na Miradi wa
Shirika hilo Nchini Tanzania Nesia Mahenge alisema changamoto iliyokubwa ni vijana kukosa
taarifa ambapo ni asilimia nne tu kati ya 3000 waliohojiwa ambao wana taarifa
za fursa zilizopo serikalini
Mkurugenzi
huyo alisema shirika hilo liliwahoji jumla ya vijana 3000 katika mkoa 6 ya Dar
es laam, Mwanza, Arusha, Mtwara, Zanzibar na Dodoma ambapo hata hivyo wamebaini
kwa sasa wengi vijana wameamka na kila mmoja ana wito wa kutaka kusimama na
kujisaidia mwenyewe katika kujiletea maendeleo
Mahenge
alisema vijana hao wanakwamishwa na ukosefu wa Ajira, Fedha za Mitaji, viwango
duni vya elimu na kutokuwa na ujuzi hali
inayowafanya kuishi kwa Hofu, mashaka na wasiwasi wa kutojua ni kwa namna gani
watatimiza malengo yao ya kimaendeleo
“vijana
hao 3000 waliorodhesha changamoto mbalimbali zinazowakwamisha huku jambo lingine
likiwa rushwa ikiwemo ya ngono
Tatizo
lililokubwa ni vijana kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu fursa mbalimbali
ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ikiwemo ruzuku za kuwezesha vijana mfono
ukiwa kwa idadi hiyo ya vijana tuliowahoji ni asilimia 4 pekee ndiyo wenye
taarifa”, alisema
Aidha
aliwataka vijana kupaza sauti ikiwemo kuwa na mijadara na serikali ili hatimaye
waweze kusaidiwa
Mgeni
Rasmi katika Kongamano hilo alikuwa Mbunge wa Jimbo la Chilonwa lililopo wilayani chamwino Mkoani humo Joel Mwaka
ambaye aliwataka vijana hao kuanzisha au kujiunga katika vikundi vilivyopo ili
iwe rahisi kwa serikali kuwaona na katimaye kuweza kuwasaidia kurahisi kuliko
kila kijana akawa kivyake ambapo hata hivyo aliwakumbusha wakuu wa wilaya na
mkoa kuitekeleza agenda ya kutenga maeneo ya ardhi kwa ajili ya vijana
Back To Top
Post A Comment: