Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza na
waandishi wa habari leo jioni katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Zainab Telack
Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Siku moja baada ya kuripotiwa kuibiwa kwa kamera mbili aina ya Canon na Stand zake mbili ikiwa ni sehemu ya vifaa vinavyotumika katika zoezi la uhakiki vyeti na kuandikisha vitambulisho vya taifa NIDA wilayani Kishapu mkoani Shinyanga,vifaa hivyo vimepatikana.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Milioni Sita vimekutwa vimehifadhiwa chini ya ardhi nyumbani kwa mmoja wa wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo jioni Jumanne Oktoba 11,2016,katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi la polisi limefanikiwa kupata kamera mbili zilizokuwa zimepotea katika jingo la halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
“Oktoba 10,2016 saa mbili asubuhi kulikuwa na taarifa za kupotea kwa kamera mbili na viegesha vyake ikiwa ni sehemu ya vifaa vinavyotukima katika zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma…..leo majira ya saa nne na nusu asubuhi tumefanikiwa kuvipata vifaa hivyo”,ameeleza Kamanda Muliro.
“Tumefanikisha kukamata vifaa hivi vikiwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wanne vikiwa vimefukiwa chini ya ardhi...yaani wamechimba shimo kisha kuvifunga kwenye mfuko na kuvifukia ardhini..hii inatokana na jeshi la polisi kuendesha zoezi la kukamata watu mbalimbali wakiwemo walinzi na wafanyakazi wa halmashauri ya Kishapu,tumekamata watuhumiwa wanne halisi wakiwemo wafanyakazi wa ndani ya ofisi wawili na walinzi wawili”,ameongeza Kamanda Muliro.
Amesema watuhumiwa wote wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi na watafikishwa mahakamani uchunguzi ukikamilika.
Post A Comment: