Katika kuelekea maazimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere octoba 14 kila mwaka, Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha (UVCCM) umeamua kuienzi kumbukumbu hiyo kwa kujitolea Damu itakayosaidia kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu
Akizungumza
katika zoezi hilo la uchangiaji damu lilofanyika katika Ukumbi wa Makao
makuu ya CCM mkoa wa Arusha Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa Zeloti Saitoti
amesema kuwa wao kama umoja wa vijana wameamau kumuenzi baba wa taifa
kwa kuchangia damu japo alituhimiza kupigana vita na maradhi, umaskini pamoja na ujinga
Akizungumza
wakati wa utoaji damu Afisa maabara kutoka Halmashauri ya
wilaya ya Arusha kitengo cha Damu salama Joseph Mpanda amesema kuwa
zoezi hili la umoja wa vijana UVCCM kujitolea damu limekuja kwa wakati
muafaka kwa maana kwa sasa hapa nchini kuna uhitaji mkubwa sana wa damu
Aidha
kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wanawake ya chama cha
mapinduzi mkoa wa Arusha (UWT) Flora Zelote ambaye alikuwa wa kwanza
kuonyesha uhamishashaji huo wa kujitolea damu amesema kuwa wao kama
jumuiya ya wazazi wameelewa umuhimu mkubwa wa kuchangia damu ndio maana wakaamua kujitokeza katika zoezi hilo
Wakati huo katibu mkuu wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Arusha chama cha Mapinduzi Agness Mchau amesema
kuwa wamekuja kushirikiana na UVCCM wao kama wanafunzi na kuwataka
vijana wote wa mkoa wa Arusha kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu
Isert SHIRIKISHO
Post A Comment: