Mfanyakazi
wa kampuni ya Hanil Jiangsu inayoshirikisha wakorea na wachina
inayofanya kazi ya upanuzi wa barabara ya kutoka Sakina-Tengeru
amefariki mara baada ya kukanyagwa na mtambo wa kushindilia barabara
unaofahamika kwa jina la Roller hapa jijini Arusha.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanasema kifo cha mfanyakazi huyo raia
wa ya China kimetokea pale ambapo mtambo huo wa barabara ulipokuwa
ukirudi nyuma ndipo ulipomparamia raia huyo na kumkanyaga.
MsumbaNEWS blog tulifika katika eneo
la Kwa Mrefu mahali ambapo tukio hili limetokea na kushuhudia umati wa
watu wakiwa eneo la hilo pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama
vikifanya juhudi za kumnasua chini ya mtambo huo ambapo alikuwa amekwama
Mara
baada ya kunasuliwa kwa mwili wa raia huyo aliyetambuliwa kwa jina la
Yao Sijiu mashuhuda wamezungumzia tukio hilo lililoleta taharuki kubwa
ambapo tukio hilo wamesema kuwa ni Mara ya kwanza kujitokeza tangu
ujenzi huo wa barabara hiyo ulipoanza.
Kwa
mujibu wa Jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia taarifa ya maandishi
limesema chanzo cha ajali ni uzembe wa opareta wa mtambo huo kutokuwa
makini na kutochukua tahadhari ya usalama wa watu wengine waliopo eneo
la kazi.
Mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa uchunguzi wa
daktari.
Post A Comment: