Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote
vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na
uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.
Uhakiki
huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote
vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa
ajili ya kufanya uhakiki huo.
Aidha,
katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote,
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi
wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za
Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya
Jumanne Oktoba 18, 2016.
Hivyo,
wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na
kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka
iwezekanavyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia
haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Post A Comment: