Fatou Bensouda wakati alipokua akila kiapo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini Hague tarehe 15 Juni 2012
Nchini
Burundi, yote yalienda kwa haraka mno baada ya serikali kuchukua uamuzi
wa kujiondoa kama mwanachama wa Mahakama ya kimataifa ya Jinai (ICC),
ikituhumiwa kuwa 'chombo cha kisiasa cha ukandamizaji.'
Baada ya
Bunge, baraza la Seneti limepiga kura kwa uamuzi wa serikali ya Burundi
wa kujiondoa kama mwanachama wa ICC na sasa ni zamu ya Rais Pierre
Nkurunziza kutia saini. Itakua ni kwa mara ya kwanza kwa mahakama hiyo,
lakini kwa uhakika, uamuzi huo hauitengi Burundi kutofunguliwa mashitaka
mbele ya mahakama ya kimataifa.
Kimsingi,
Mahakama ya Kimataifa haiwezi tena kuchunguza kwa jitihada zake nchini
Burundi, mara tu mwaka mmoja utakua umemalizika baada ya nakala hiyo
kutiliwa saini na rais wa Burundi. Hata hivyo uamuzi huo hautoitenga
Burundi kutofuatiliwa na mahakama ya kimataifa. Inatosha tu kwamba
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuruhusu nchi hiyo kufuatiliwa na
mahakama ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa kesi ya Darfur mwaka 2005 na
Libya mwaka 2011.
Jumuiya
ya kimataifa pia imeweka wazi kesi ya wanachama ambao wataamua kujiondoa
katika ICC ili kuepuka mashtaka, mtaalamu aliyehojiwa na RFI ameeleza.
Sheria za Roma zinaeleza kwamba 'uamuzi wa kujiondoa ICC unachukua mwaka
mmoja baada ya tarehe ambayo uamuzi huo utakua umewasilishwa kwa vyombo
husika,' uamuzi wa kujiondoa hautakua na athari kwa kesi ambazo tayari
zinaendelea kushughulikia na taasisi hiyo ya kimataifa hata kama uamuzi
huo utasahihishwa.
Mwendesha
mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda, alizindua mwezi April mwaka huu
uchunguzi wa awali kuhusu mauaji, mateso na ubakaji nchini Burundi.
Wakati huo huo, kundi la wanasheria liliwasilisha kwa Mahakam ya
Kimataifa ya Jinai (ICC) tangu miezi mitatu iliyopita kesi ya waathirika
zaidi ya mia moja au warithi wa waathirika wa unyanyasaji huo.
Hatimaye,
na hii pengine ni moja ya sababu iliyopelekea serikali ya Burundi
kuchukua uamuzi wa kujiondoa katika ICC: baraza la Haki za Binadamu la
Umoja wa Mataifa liliamua, siku chache tu zilizopita kuunda tume ya
uchunguzi wa kimataifa kufuatia ripoti ya wataalam iliyohusisha serikali
ya Burundi katika uhalifu mkubwa. Orodha ya wahusika katika uhalifu huo
tayari imewekwa wazi.
Back To Top
Post A Comment: