Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.
Uamuzi
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea
maeneo yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na
Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.
“Hii
si mara ya kwanza kwa mashabiki kuvunja mageti na kung’oa viti na sisi
kama Serikali tumeamua kuzuia vilabu hivi vya Simba na Yanga kutotumia
Uwanja wa Taifa mpaka tuitavyoamua vinginevyo hapo baadae” Alisistiza
Mhe. Nnauye.
Mhe.
Nape Nnauye ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani
ili kubaini makosa yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya
kihualifu na uharibifu katika Viwanja vya michezo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex
Nkenyenge amesema kuwa wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika
mechi ya Simba na Yanga na kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya
kuingilia Uwanjani.
Ameongeza
kuwa kwa tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki
kwa upande wa Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti
1781 vimeng’olewa katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara
nyingi tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya
watanzania wote na kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki
kilichotokea na tujue kuwa ni kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga
Uwanja huu na pia ndizo zitazotumika kukarabati Uwanja tuwe na tabia ya
kupenda na kutunza vya kwetu.
Klabu
za Simba na Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania
na kumekuwa kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutana
ikiwemo uharibifu wa miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki
pale mmoja wao anapofungwa.
Waziri
wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuzuia timu za Simba na
Yanga kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu
uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa
Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akiwa amekaa
akiangalia jinsi viti vilivyong’olewa katika Uwanaja wa Taifa na
Serikali kuchukua
uamuzi wa kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa na
kuzuia mapato ya mechi waliyocheza mpaka watakapolipa fidia kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri
wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama
moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na
Serikali kufikia uamuzi
wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa
miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu tathimini iliyofanyika mara baada ya
mechi wa jana kati ya Simba na Yanga na jumla ya mageti manne yamevunjwa
na viti1781 vimeong’olewa katika Uwanja wa Taifa.
Posted by Imma msumba
Post A Comment: