Tarehe
18-10.2016 saa 10;00 jioni maeneo ya Salasala Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni Polisi wakishirikiana na Kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa
miondo mbinu ya Shirika la umeme Tanzania
Tanesco lilipata taarifa toka
kwa raia mwema kuwa kuna watu wanaohujumu miundo mbinu ya Shirika hilo.
Kikosi
hicho kilifika eneo hilo katika nyumba ya Willfred Barutti (45) mkazi
wa Makumbusho na kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo ambapo walivipata
vifaa mbalimbali Line Meterial ambavyo hutumika kwa ajili ya kuunganisha
umeme vya Kampuni ya Tanesco.
Polisi
waliwenda katika nyumba nyingine mali ya Betrice Emmanuel (42) mkazi
wa Salasala Mabanda wakafanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa
vifuatavyo;
Nyaya
aina yka Drums'02,roller ya waya aina ya AICC ya umeme wa 50 mm ambazo
hutumiwa na tanesco kituo cha Kilimahewa huko Kawe Wilaya ya Kinondoni
Thamani
ya vifaa hivyo vinakadiliwa kuwa Tsh.61,000,000,Watuhumiwa wawili
wanashikiliwa kwa mahojiano na Upelelezi utakapokamilika tapelekwa
mahakamani kwa hatua za kisheria.
Post A Comment: