Pichani : Scorpion, mwenye fulana nyekundu, akiwa mahakamani jana chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Jana katika mahakama ya
wilaya ya Ilala, mkazi wa buguruni kwa mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma
watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama
Scorpion amepandishwa kizimbani na kusomewa tena shtaka la unyang’anyi
wa kutumia silaha .
Kesi ya Scorpion, ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha
kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa mabibo Hostel, inasikilizwa na hakimu
Adolf Sachore.
Leo kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka
umeieleza mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na
hivyo mtuhumiwa amerudishwa rumande.
Back To Top
Post A Comment: