Jina lake halisi ni Salim H Njwete au
Samjet. Unaweza ukawa umewahi kumuona sehemu. Mwaka 2012, alikuwa
mshindi wa shindano la Dume Challenge lililowakutanisha vijana 20 wababe
wa mazoezi na kazi ngumu. Salim alijinyakulia kitita cha shilingi
milioni 20.
Salim Njwete aka Scorpion (Kushoto)
akikabidhiwa mfano wa hundi kufuatia kutangazwa mshindi wa shindano la
Dume Challenge, December 2012
Ni mwalimu wa karate na mbabe wa
mapigano na ndio maana pindi anamshambulia Said hakuna aliyethubutu
kumsaidia kwasababu kila mtu maeneo ya Buguruni anamhofia.
Ni muigizaji wa filamu pia na kwa mujibu
wa Walter, aliyekuwa mshiriki mwenzake kwenye Dume Challenge, baada ya
mashindano hayo Salim alitoa filamu moja.
Alivyokuwa
Mdogo Alikataa Kusoma Mama Yake Mzazi Alishafariki Siku Nyingi Na
Alikuwa Akilelewa Na Mama Yake Mdogo Maeneo Ya Yombo Buza.
Alishawahi
Kufungwa Jela Japo Haijajulikana Alikosa Nini, Na Jina Lake Kamili Ni
Salum Njwope Na Jina Hilo Nila Babu Yake. Yeye Ni Mwenyeji Wa Mkoa Wa
Shinyanga. Kwa Mujibu Wa Mama Yake Mdogo Anasema Scorpion Alipokua
Akitoka Nyumbani Usiku Saa Mbili Anamuaga Mama Yake Mdogo Huyo Kuwa
Anakwenda Kwenye Kazi Ya Ubaunsa Katika Club Kumbe Mwenzie Alikuwa
Anaenda Buguruni Kuibia Watu Mpaka Asubuhi Ndio Anarudi Nyumbani.
Pia
Scorpion Ashawahi Kushiriki Katika Shindano Lililojulikana Kama Dume
Challenge Kama Miaka Mitatu Iliyopita Na Aliibuka Mshindi. Napia Alianza
Mafunzo Ya Kucheza Caret Tangu Akiwa Mdogo Sana Napia Ni Mtu Mwenye
Nguvu Za Kuzaliwa Nazo.
Kuna
Kipindi Aliondoka Nyumbani Kwao Kwa Muda Mrefu Mama Yake Mdogo Anadai
Alikuwa Hajui Yuko Wapi Mpaka Baadae Aliporudi Mwenyewe Nyumbani.Amekamatwa
Na Polisi Baada Ya Kutuhumiwa Kumjeruhi Mkazi Mmoja Wa Dar Es Salaam
Eneo La Buguruni Kwa Kumng’oa Macho Katika Kitendo Kilichoelezwa Kuwa Ni
Wizi Wa Fedha.
Back To Top
Post A Comment: