Jeshi la mkoani Arusha linawashikilia watu Wa nne akiwemo
mmiliki Wa Kambi ya LILAC inajishulisha na maswala ya utalii mto Wa mbu
John Kadozo(46) mwenye asili ya kiasia mkazi Wa mto Wa mbu wilayani
Monduli kwa kosa la kumchoma kwa kumwagia petroli mfanyakazi wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda Wa Polisi mkoa
Wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea October 9
majira ya saa nne Usiku ndani ya Kambi ya mtuhumiwa iliopo mto Wa mbu
wilayani Monduli.
alisema kuwa mtumiwa alimchoma moto mtoto aliyejulika kwa
jina la Paskali Alfonce (17) mkazi Wa mto Wa mbu aliyekuwa mpishi Wa
kampuni yake kwa kosa la kuchelewa kubandika maharage.
"Inasemakana kijana huyu alikuwa mpishi Wa pale sasa Siku
hiyo alipewa fedha akanunue maharage alipoenda alichelewa kurudi ndipo
mtuhumiwa na wenzake walipomkamata kijana Huyo na kumwagia petroli kisha
kumuwasha "alisema mkumbo
Aliwataja watuhumiwa wengine ambao walishirikiana kufanya
tukio hilo na wote wana shikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni John Kadozo
(46),George Kessy (28) Martin Petro (16) Enock Wilium (19) na
watuhumiwa wote wapo mahabusu na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
mapema iwezekanavyo .
Akisimulia tukio niko kwa uchungu mtoto Alfonce ambaye
amelazwa katika hospitali Seliani iliopo ngaramtoni alisema siku hiyo
alitumwa maharage ila alichelewa kurudi kutokana na kuyakosa lakini
aliporudi ndipo walipomkamata na kumfunga shuka mikono wakamwagia
petroli kisha kumchoma
"Nilibahatika kuchoropoka nikakimbia sasa Jirani Hapo
kunamfereji nika rukia uko ndio nikazimika maana niliwaka kabisa
"alisema mtoto Alfonce
Akilia kwa uchungu mama mlezi aliyejitambulisha kwa jina la
Cristina Faustine alisema anasikitika sana maana Amemlea uyo toto kwa
shida tangu wazazi wake wafariki na aliamua amruhusu kwenda kufanya kazi
ili aweze kujikimu na aweze kujipatia maitaji yake.
Aidha alitumia muda huo kuiomba serekali kuakikisha mtoto
uyo anapata matibabu na kwani kwasasa anauwezo wakugaramia matibabu ya
uyo mtoto.
Post A Comment: