Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wakazi wa Kanyonza Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, alipokagua maendeleo
ya ujenzi wa barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia)
akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza (kulia),
inayojenga barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 mkoani
Kigoma. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa
wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiangalia
nodo zinazoshikilia moja ya madaraja yanayojengwa katika barabara ya
Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 mkoani Kigoma.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoka
kukaguzi wa moja ya madaraja yanayojengwa kwenye barabara ya
Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 mkoani Kigoma.
Muonekano wa kalvati katika barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 mkoani Kigoma.
Muonekano
wa barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 mkoani Kigoma.
Barabara hiyo kwa sasa imefikia asilimia 18 ya ujenzi wake.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi
minne Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works kuongeza kasi ya ujenzi wa
barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 kukamilika kwa
wakati na wananchi wa Kibondo na maeneo ya jirani kuweza kuitumia.
Waziri
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wilayani Kakonko mkoani Kigoma mara
baada ya kukagua barabara hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake.
“Mwezi wa
pili mwakani nitarudi hapa kukagua tena maendeleo ya ujenzi wa barabara
hii sababu bado kasi mnayokwenda nayo hainiridhishi na kampuni hii ni
ya kizalendo ambayo ilitakiwa kuwa ya mfano”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri
Mbarawa amemsisitiza mkandarasi huyo kuzingatia viwango bora vya ujenzi
wa barabara kama ilivyosainiwa kwenye mkataba na kumtaka kuzingatia
thamani ya fedha katika ujenzi anaoufanya.
“Rafiki
yangu ni yule anayefanya kazi vizuri hata kama awe mwanangu kama hafanyi
kazi vizuri nitamfukuza”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Naye,
Mkandarasi wa kampuni hiyo Bw. Atul Ramji ameahidi kutii na kulifanyia
kazi agizo la waziri huyo na kusema kuwa ifikapo mwezi wa pili mwakani
ujenzi utakuwa umepiga hatua kubwa.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),mkoa wa
Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi wa barabara hiyo kwa sasa
umefika asilimia 18 kutoka asilimia tano zilizokuwepo awali ambapo kwa
sasa kazi zinazofanyika ni ujenzi wa makalvati katika barabara hiyo.
Katika
hatua nyingine Waziri Mbarawa amemuagiza mkandarasi wa kampuni hiyo
kuanza mara moja kuipatia huduma ya maji Shule ya Sekondari ya Kanyonza
angalau mara moja kwa wiki kutoka kwenye kambi ya ujenzi wa barabara
wakati Serikali ikiendelea kutafuta suluhisho la kudumu.
Prof.
Mbarawa amechukua hatua hiyo baada ya wananchi wa kijiji cha Kanyonza
kumsimamisha na kumueleza changamoto ya Shule ya Sekondari hiyo iliyopo
katika kijiji hicho wilayani Kakonko kukabiliwa na uhaba wa maji hali
inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali wa zaidi ya kilometa nne kufuata
huduma hiyo.
Post A Comment: