POLISI
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imefanya operesheni katika maeneo ya
katikati na pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam na kuwakamata watuhumiwa
87 wa makosa mbalimbali, wakiwemo waliokuwa kwenye mtandao wa uhalifu
wa mkazi wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34)
maarufu kama ‘Scorpion’.
Njwele
alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwishoni mwa wiki,
kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote
mawili Said Mrisho.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda
hiyo, Kamishna wa Polisi Simon Sirro alisema watuhumiwa wengine
wanadaiwa kuvunja nyumba na kuiba na wengine walipatikana na gongo lita
148, bangi kete 95 na puli 48.
Alisema
watuhumiwa hao, wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya
Mbagala, Buguruni, Kiluvya, Gongo la Mboto, Tandika, Ukonga, Banana,
Kunduchi, Keko, Kawe.
“Watuhumiwa
hao walipatikana na makosa mbalimbali yakiwemo kuvunja nyumba usiku na
kuiba maarufu 10 ndani 10 nje, kuvuta na kuuza bhangi, kuuza na kunywa
gongo, kupiga debe, uzembe na uzururaji,” alisema Kamanda Sirro.
Post A Comment: