Mkuu wa
Mkoa wa Arusha (mbele kulia) akikagua ujenzi wa barabara ya Friends
corner –Muriet inayojengwa kwa kiwango cha Lami kupitia mradi wa Mpango
Mji Mkakati (TSCP) unaotekelezwa na Tamisemi. Barabara hiyo itajengwa
kwa urefu wa Km 6.5
Kupitia
Ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisikiliza kero za wananchi wa
eneo la soko Mjinga Kata ya Sokoni 1 ambapo kero kubwa ilikuwa ni
kufungwa kwa barabara kutokana na ujenzi holela
Kutoka
Kulia ni Mhandishi wa Ujenzi Jiji Eng. Gaston Gasana akifuatiwa na
Mhandisi Mshauri wa Mradi wakielezea kazi zitakazofanyika katika Mradi
huu.
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) akiskiliza taarifa ya kazi
zinazoendelea katika Dampo la kisasa la Muriet toka kwa Afisa Usafishaji
wa Jiji Bw. James Lobikoki
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kushoto) akihoji kuhusu zabuni za
ujenzi wa barabara ya Oljoro – Muriet kwa Afisa Manunuzi wa Jiji Bw.
Seif Kasori(kulia). Mkandarasi anayejenga barabara hiyo toka kampuni ya
Surchet Building and Civil works yuko nyuma ya muda na ametakiwa
kukamilisha kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.
Lyidia Kishia Arusha
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,
Athumani Kihamia kuchunguza kwa undani juu ya zabuni aliyopewa mkandarasi anaye jenga Barabara katika barabara ya Oljoro /Murriet Jijini
hapa.
Gambo ametoa agizo hilo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja ya
kukagua ujenzi wa Barabara ya Friends corner – Muriet inayojengwa Kwa
kiwango cha Lami na mradi wa Mpango Miji Mkakati ( Tanzania Strategic
Cities Project) unao tekeleza Na Tamisemi pamoja Barabara hiyo ya
Oljoro – Muriet inayojengwa Kwa kiwango cha Changarawe kwa Fedha za
mapato ya ndani ya Halmashauri.
Amesema amegundua kasoro Kwa Kampuni ya Surchet Building and Civil works
inayojenga Barabara ya Oljoro Kwa kuwa Mkandarasi yuko nyuma ya muda
Na huenda asimalize kazi Kwa wakati. Pia dhamana ya Utekelezaji wa
Mradi aliyoweka Ni kubwa kulinganisha na inayotakiwa hali hii inaonyesha
kuwa zabuni hiyo ilitolewa Kwa mianya ya rushwa au dhamana hiyo Ni
feki.
Kwa
kawaida Dhamana ya Utekelezaji wa Mradi ( Perfomance bond) huwa Ni 10%
Mpaka 15% ya Gharama ya Mradi lakin mkandarasi huyu amewasilisha 30% je
dhamana hiyo ni halali kweli kwanini alete kiasi kikubwa zaidi ya
kinachohitajika huenda Ni batili Ndio maana hana uchungu nayo na Mpaka
sasa kazi iliyokamilika Ni ya ujenzi wa Mifereji tu sasa kupitia Ziara
hii nahitaji uchunguzi wa kina ufanyike Na kazi hii ikamilike ndani ya
muda wa mkataba alisema Gambo.
Barabara
ya Oljoro Muriet inajengwa Kwa urefu wa Km 2.6 sambamba Na Mifereji ya
kusafirishia maji yenye urefu km 1.1, Gharama Za Mradi Ni Tsh Mil 157.8
Na Barabara hii inategemewa kukamilika Mwishoni mwa Mwezi Oktoba 2016.
Post A Comment: