Jeshi la Polisi Mkoani KAGERA limethibitisha kumshikilia na kumhoji Mbunge wa jimbo la BUKOBA Mjini WILFRED LWAKATARE kwa tuhuma za kuandika barua ya kuomba misaada kwa wafadhili  mbalimbali ,kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani humo Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA AUGUSTINO OLLOMI uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo bado unaendelea .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA AUGUSTINO OLLOMI amethibitisha jeshi la Polisi Mkoani KAGERA kumshikilia na kisha kufanya mahojiano na Mbunge huyo ambaye anatuhumiwa kuandika barua kwenda kwa wafadhili mbalimbali kuomba misaada kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi huku akijua kuwa suala hilo linaratibiwa na Kamati ya maafa ngazi ya taifa  pamoja na kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa kamanda huyo wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA Mbunge  LWAKATARE anadaiwa kuandika barua iliyoelekeza misaada ya fedha kutumwa katika namba ya simu  ambayo mmiliki wake naye anashikiliwa na jeshi hilo.

Hata hivyo uchunguzi juu ya tuhuma hizo bado unaendelea na kwa sasa mbunge huyo ameachiwa ili ahudhurie vikao vya bunge vinavyotarajia kuanza  mjini Dodoma.

Wakati huo huo wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kupitia kwa Mkuu wa mkoa wake SAID MECKY SADICK amekabidhi zaidi  ya shilingi milioni mia moja na sita kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi, na kuwataka waathirika a tetemeko hilo kuwa watulivu

Share To:

msumbanews

Post A Comment: