Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema azua
tafrani kwenye uzinduzi wa hospitali ya mama na mtoto jijini Arusha
Picha kushoto mbunge wa jimbo
la Arusha mjini Godbless Lema akitulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,wa
kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza
katika uzinduzi huo
Mwananchi
aliyehudhuria katika uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto
ambaye hakupenda kutaja jina lake akimuomba mbunge wa jimbo la Arusha
mjini Godbless Lema kutulia na kumuacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa
hutuba.
MKUU wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemumbua mbunge wa jimbo la Arusha Mjini
Godbless Lema wakati wa uzinduzi wa hosptali ya mama na mtoto katika
eneo la Bruka lililopo wilayani Arumeru .
Gambo
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa
hosptali hiyo aliishukuru kampuni ya mawakili ya Mawala (Mawala Advocate
)kwa kutoa eneo hilo kwa ajili ya hosptali hiyo ambayo ujenzi wake
umefadhiliwa na taasisi ya Martenity Africa.
Mara
baada ya Rc. Gambo kutoa kauli hiyo Lema alisimama na kuanza kupiga
kelele akidai kuwa kiwanja hicho amekitafuta yeye jambo ambalo siyo
kweli kwani kiwanja hicho kilitolewa na kampuni hiyo ya uwakili.
Hata
hivyo Rc. Gambo alilisitiza kuwa eneo hilo awali lilikuwa mali ya
kampuni ya uwakili ya mawala ambayo ilitoa eneo hilo kwa ajili ya
kujenga hosptali ya kutoa huduma kwa mama na mtoto.
“Kwa
niaba ya serikali naishukuru sana kampuni ya mawala ambayo imetoa eneo
hili kwa ajili ya ujenzi wa hosptali hii ambayo ina umuhimu mkubwa”
Akizindua
ujenzi huo ambapo alikuwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Arumeru
Alexander Mnyeti Gambo aliwahakikishia wafadhili hao kuwa serikali iko
pamoja nao katika ujenzi wa hosptali hiyo ili kuwezesha kutoa huduma
bora kwa wanannchi.
Ukweli
huo ulionekana kumkera Lema na kuonekana kuwa ameumbuka na kudai kuwa
ardhi hiyo ameitafuta yeye jambao ambalo lilipuuzwa na uzinduzi
ukaendelea kama kawaida.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa taasisi ya Martenity Africa Mchungaji Prf.
Wilfred Lau alisema taasisi hiyo imekusudia kujenga hosptali hiyo lengo
likiwa ni kusadia mama na mtoto haswa tatizo la Fistula linalowakumba
kina mama wengi wajawazito.
Kwa mujibu Prf. Lau alisema mradi huo kwa hatua ya kwanza utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni mbili.
“Mradi
huu awamu ya kwanza utagharimu dola za kimarekani milioni mbili na
ukikamilika tutatoa elimu kwa wakunga jinsi ya kuwakinga kina mama
wajawazito na ugonjwa wa fistula”.
Alisema
hosptali hiyo itakoa maisha ya kinamama wengi kutoka maeneo ya vijijini
kutokana na wakunga katika maeneo hayo kutokuwa na elimu ya kutosha juu
ya kudhibiti ugonjwa huo wa Fistula.
Post A Comment: