MANISPAA ya Songea Mkoa wa Ruvuma
kuanzia sasa imepiga marufuku vitendo vya upigaji picha wodini kwa
kutumia kamera au simu za mkononi katika hospitali na vituo vyake vyote
vya afya.
Manispaa ya Songea inatekeleza agizo la Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma
ambalo ni agizo la Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto ambalo linaeleza kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi kupiga picha
wodini wanapofika kuwajulia hali ndugu zao ambapo baadhi ya picha
wanazopiga zimekuwa zinaoneshwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na
ujumbe wenye kupotosha jamii.Hata hivyo wakurugenzi wanatakiwa
kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuwasilisha malalamiko yao inapotokea
ukiukwaji wowote katika utoaji huduma za afya.
Back To Top
Post A Comment: