Nyota wa televisheni nchini Marekani Kim Kardashian alishambuliwa na kuzuiliwa na watu waliokuwa na silaha katika hoteli moja mjini Paris, taarifa zinasema.

Msemaji wake anasema nyota huyo wa uigizaji wa vipindi vya maisha ya uhalisia alizuiliwa na watu waliokuwa wamejifanya maafisa wa polisi.

"Ameshtushwa sana na tukio hilo lakini hajaumizwa," msemaji wake amesema.

Mumewe Kanye West amekatiza ghafla tamasha ambayo amekuwa akishiriki mjini New York.

BBC

Share To:

msumbanews

Post A Comment: