Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa wingi wa kura limemteua aliyekuwa waziri mkuu wa Ureno Antonio Guterres kuwa katibu mkuu mpya wa umoja huo.

Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kufanyika wiki ijayo kuidhinisha uchaguzi wake kwa muhula wa miaka mitano.

Bwana Guterres ,mwenye umri wa miaka 67,ambaye aliongoza kitengo cha wakimbizi katika Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka 10 atachukua mahala pake Ban Ki-moon mapema mwaka ujao.

Bwana Ban mwenye umri wa miaka 72,alimtaja bwana Guterres kama 'chaguo zuri' la kumrithi.

''Uzoefu wake kama waziri wa Ureno, ujuzi wake wa maswala tofauti duniani na ukakamavu wake utamsaidia katika kuliongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika kipindi muhimu'' ,bwana Ban aliwaambia wanahabari alipozuru mjini Rome.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: