Home
BURUDANI
Habari Kuhusu Kuvunjika Kwa Kundi la Muziki la Yamoto Band
Msimamizi wa Yamoto Band, Chambuso, ameweka wazi kuwa fununu
zinazoendelea juu ya kundi hilo la muziki kutoelewana kwa sasa siyo za
ukweli.
Akizungumza na eNewz, Chambuso amesema kuwa Yamoto Band kwa sasa wamekua
na kwamba wana uamuzi wa kufanya vile wanavyo jisikia na suala la
nyumba walizojengewa ni za kwao hata kama hawataendelea kufanya kazi na
Said Fella.
“Tukianza nao walikuwa watoto kuna vitu tulikuwa tukiwazuia wasifanye
hata kuzurura mitaani kuna kipindi tulikuwa tukiwazuia lakini kwa sasa
wameshakua na wanamaamuzi ya kufanya mengi ndiyo maana unaona kwa sasa
Asley anapost ana mtoto hiyo ni ishara ya kuonesha kuwa wameshakua”
Alisema Chamuso.
Akimalizia amesema kwa sasa mashabiki wasubirie ngoma mpya na video
nzuri kutoka kwa Yamoto Band kwa kuwa hamna tatizo lolote na uongozi wao
na hakuna tatizo lolote baina yao.
Back To Top
Post A Comment: