Hit maker wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amemtaja Ne-Yo,
WizKid, Tekno pamoja na Flavour kuwa ni miongoni mwa mastaa walioukubali
wimbo wake mpya ‘Salome’.
Muimbaji huyo amedai kila mmoja kwa wakati wake alivyoona video ya wimbo huo, alionesha kupendezwa na kile alichokifanya.
“Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania wakati nipo naye
nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, “Diamond alikiambia kipindi cha
FNL cha EATV.
“Hata baada ya wimbo kutoka wasanii wakubwa kama akina Tekno, Flavour
walinitumia ujumbe mfupi kuonyesha kupenda, nakumbuka hata Ne-Yo naye
aliniambia ‘I like the song.
Post A Comment: