Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba
akizungumza katika uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa
wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam
(DAWASCO) Mkoani Pwani
Mwenyekiti
wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu
Samwel Kitundu akizungumz machche kwenye uzinduzi wa Semina ya pamoja ya
mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar
es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba pamoja
na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja
Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu wakiwa kwenye picha ya pamoja na DAWASCO
na DAWASA Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati amezindua Semina ya pamoja
ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini
Dar es salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es
salaam (DAWASA) iliyofanyika mjini Bagamoyo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Mfutakamba amezitaka taasisi hizo kuongeza
ushirikiano,haswa kwa wafanyakazi kwa kuwaandalia semina za mafunzo kwa
pamoja ili waweze kufahamiana na kushirikiana kwa pamoja katika kuondoa
kero ya Maji iliyopo jijini Dar es salaam.
“Mimi
faraja yangu ni kuona DAWASCO na DAWASA mnashirikiana haswa wafanyakazi
kwa kuwa kitu kimoja katika kutimiza majukumu yao, muone tatizo la Maji
ni lenu wote ,naamini mkipendana na kuwa wamoja mtasaidia sana kuondoa
kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam” alisema Mfutakamba.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA Meja
Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu amemshukuru katibu mkuu kwa kufika na
kuzindua semina hiyo na pia amewataka washiriki hao kutumia elimu
watakayopata kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na kutatua
kero ya Maji kwa jiji la Dar es salaam.
“Kwa
niaba ya DAWASCO na DAWASA tunakushukuru katibu mkuu kwa kuweza
kushiriki nasi kuzindua semina hii ya mafunzo kwa wafanyakazi wa taasisi
hizi mbili tunaona upo pamoja nasi hivyo na mimi napenda kuwa sisitizia
washiriki wa semina hii kutumia elimu na ujuzi watakaopata kuboresha
huduma ya Maji kwa kuwa wabunifu kwenye maeneo yao ya kazi nakuondoa
kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa
pwani” alisema Kitundu.
Post A Comment: