Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali. Ukweli wafahamika baada ya mara kadhaa rapper Young Dee kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano na video vixen kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.

Akiongea na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka ukweli kwa kusema kuwa amekuwa na mahusiano na rapper huyo kwa tangu miaka minne iliyopita wakati akiwa mkoani Mbeya.

Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi naye, mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio nilienda kumtoa ndugu zake wote walikataa kwenda, Mimi nimeenda. Matatizo yangu yeye anayafurahia ina maana. Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni mtu ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,amesema Amber.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: