WAFA KWA KUKOSA HEWA MGODINI.

 Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa.

 
Watu watatu waamefariki dunia baada ya kukosa hewa walipokuwa wakichimba dhahabu katika mgodi unaomilikiwa na Soda Wilson Mziuli (68)mkazi wa kijiji cha Itumba Kata ya Chalangwa tarafa ya Chalangwa Mkoa wa Mbeya. 

 Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amewataja waliofariki kuwa ni Zawadi Soda  (28, Wilson Soda (24)na Jamali Omary(20) na kwamba wachimbaji hao walikumbwa na mauti September 17 mchana . 

Madusa amesema chanzo cha vifo hivyo ni kukosa hewa baada ya mashine ya kuingiza hewa(copressor)kushindwa kufanya kazi hivyo kusababisha maji katika mgodi huo unaokadiriwa kuwa na urefu wa mita 50 kwenda chini.

 Baada ya juhudi kubwa kufanyika miili ilipatikana na kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi. Aidha ametoa wito kwa wachimbaji na wamiliki kufuata taratibu na tahadhari za kiusalama ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika. 

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Chunya  aliufunga mgodi mmoja wa mwekezaji eneo la Matundasi  kwa kukiuka taratibu za usalama kazini na kusababisha kutiririsha maji yenye sumu  kwenye makazi ya watu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: