Home
SIASA
Wafuasi wa Profesa Lipumba Wakusanyika Makao Makuu ya Cuf wakisubiri kumpokea kama Mwenyekiti
Vikundi vya wafuasi Profesa Ibrahim Lipumba wamekusanyika
katika Ofisi za CUF Buguruni wakisubiri kumpokea mwenyekiti huyo wa
zamani na kumwingiza ofisini.
Wanachama hao wanadai wana barua ya Msajili wa vyama vya siasa inayomtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti halali wa CUF.
Mwandishi wa Mwananchi, Ephrahim Bahemu aliyeko kwenye eneo
hilo anasema geti la ofisi za CUF limefungwa na ndani hakuna kiongozi
yeyote wa chama.
Bahemu anasema mashabiki hao wa Lipumba wanaoimba na
kucheza, wanasema msafara wa Profesa uko njiani kuelekea kwenye ofisi
hizo za makao makuu ya chama hicho.
Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya
Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amesema ndio wamepokea barua ya msajili
na bado wanaisoma ili kuona imeelekeza kitu gani.
Hata hivyo, Mtatiro amesema kwa vyovyote vile msajili wa
vyama vya siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya chama
chochote cha siasa.
Back To Top
Post A Comment: