Home
SIASA
Waandamana tena Marekani kupinga mauaji
Waandamana tena Marekani kupinga mauaji
Mamia ya waandamanaji wamekusanyika
kwa usiku wa tatu mfululizo, kwenye mji wa Charlotte Marekani kufuatia
kuuawa kwa mtu mweusi akiwa mikononi mwa polisi.
Wengi wanataka kutolewa video inayoonyesha mwanaume huyo akipigwa risasi.
Polisi wameionyesha familia ya marehemu video, hiyo lakini wakasema kuwa hawataitoa kwa umma.
Mkuu
wa polisi katika mji wa Charlotte anasema video hiyo haionyeshi kuwa
Keith Lamont Scott alikuwa na bunduki mkononi wakati aliuawa.
Familia yake nayo inasema kwa ni vigumu kutambua alichokuwa nacho mkononi wakati huo.
Back To Top
Post A Comment: